Adama Barrow amteua Fatoumata Jallow-Tambajang kuwa makamu wa Rais wa Gambia

0
248

Rais wa Gambia, Adama Barrow amemteua Fatoumata Jallow-Tambajang kuwa makamo wa rais ambaye amekidhi vikezo vya kuwa na umri miaka 65.

Fatoumata Jallow-Tambajang mwenye ushawishi mkubwa ambaye aliwahi kuwa mshirika wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh kabla ya kujiunga na upinzani ulioshinda uchaguzi kuwa makamu wake wa urais.

Lakini watu wanatilia shaka iwapo bi Tambajang mwenye umri wa miaka 68 anahitimu kupewa wadhfa huo kutokana na umri wake.

Tambajang amewahi kuhudumu kama waziri wa afya na maswala ya kijamii wakati wa utawala wa Yahya Jammeh lakini akalazimika kwenda mafichoni baada ya kukosana naye.

Baadaye alikuwa kiungo muhimu katika kuanzisha upinzani uliomshinda Jammeh kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba mwaka jana.

LEAVE A REPLY