Mtayarishaji na muongozaji wa ‘video’ za muziki wa bongo fleva nchini, Adam Juma amesema ataacha kujishughulisha kazi hiyo ndani ya muda mfupi ujao.

Hayo yametokana na baadhi ya wasanii kudai mkongwe huyo kuishiwa ubunifu mpaka kupelekea waandaji chipukizi kuwa gumzo mjini.

 “Mimi nimepumzika na sitaki kufuatilia mambo hayo ya muziki kila mtu ana misimamo yake na kwa sasa nataka niache kabisa mambo ya muziki nataka nifanye mambo yangu mengine ni ‘relax’ na kama kuna mtu anahisi mimi ni mjinga au mpumbavu ‘it’s fine’.

Katika tasnia ya bongo fleva pamekuwa na kawaida kwa wasanii waliotoka na kupiga hatua fulani kimuziki kutowathamini wale watayarishaji walioweza kuwa’push’ hatimaye jambo ambalo huwafanya watayarishaji hao kuvunjika moyo katika kazi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *