Chama cha ACT – Wazalendo kinatarajia kumualika kiongoizi wa chama cha Economic Freedom Fighter cha Afrika Kusini, Julius Malema kuhudhuria mkutano unalenga kujadili mustakbali wa lililokuwa Azimio la Arusha.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu ametaja vyama vingine vilivyoalikwa na ambavyo viongozi wake wanatarajiwa kuwasili nchini kuwa ni chama cha Labour cha nchini Uingereza, Die Link cha nchini Ujerumani na Syriza kutoka nchini Ugiriki.

Shaibu amesema wakiwa nchini, viongozi hao watashiriki mjadala mpana wa maudhui ya lililokuwa Azimio la Arusha ambalo hivi karibuni ACT Wazalengo imeliibua upya na kuliita Azimio la Tabora, ambayo kimsingi maazimio yote yanazungumzia ujenzi wa jamii inayochukia rushwa na aina zote za unyanyasaji huku ajenda kuu ikiwa ni ujamaa na utaifa kwanza.

Chama cha ACT – Wazalendo kinatarajia kuandaa mkutano huo kwa ajili ya kujadili mustakabali wa Azimio la Arusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *