Mwenyekiti wa kamati ya pili iliyofanya uchunguzi wa usafirishaji wa mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro amesema kuwa kampuni ya madini ya Acacia haina sifa ya kufanya shughuli za uchimbaji wa madini hapa nchini.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kampuni hiyo ya uchimbaji madini nchini ambayo inamiliki migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi haijasajiliwa nchini.

Hayo yamesemwa leo wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya pili kuhusu usafirishwaji wa machanga wa madini mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo inayowasilisha ripoti yake leo iliteuliwa na Rais na ilipewa adidu mbalimbali ikiwemo kufanya tathmini wa usafirishaji wa mchanga huo iwapo iwapo ilizingatia mikataba MDA’s na kuangalia kama maslay ya wananchi yamezingatiwa katika mikataba hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *