Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abukakari Mzuri amefunguka na kusema kuwa yeye siyo Marioo kama ambavyo watu wamekuwa wakisema kuwa analelewa na mwanamke au ameolewa na mwanamke.

Abubakari Mzuri amesema kuwa yeye hajaolewa wala halelewi na mwanamke bali anaishi na mwanamke huyo na kwamba yeye ndiye anayemuhudumia kwa kuwa mwanamke huyo hana kazi yoyote anayofanya.

Abubakar amesema kuwa “Unajua mimi huyo ni mwanamke niliyekuwa naye mwanzo na sasa nimerudiana naye na kuna tetesi kuwa mimi sijui Marioo mimi siyo Marioo bali naishi na huyu mwanamke hapa hata yeye atasema hapa, baada ya vurugu kutokea hapa nimemletea nini ndani mimi siyo Marioo”.

Kwa upande wa mwanamke ambaye anadaiwa kumlea Abubakari Mzuri alikana yeye kumlea msanii huyo ingawa maelezo yake yalikuwa wazi kuwa yeye ndiye mmiliki wa vitu vingi ndani ya nyumba hiyo ambayo sasa wanaishi pamoja amesema kuwa yeye na Mzuri ni wapenzi na wala amlei kama watu wanavyosema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *