Kiungo wa zamani wa Simba SC na Azam FC, Abdulhalim Humud amejiunga na klabu ya Real Kings FC ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini.

Humud ambaye msimu uliopita alichezea Coastal Union ya Tanga iliyoshuka daraja katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na timu ya hiyo.

Real Kings walipanda Ligi Daraja la Kwanza mwaka huu na wakafanikiwa kufika fainali ya ligi ya ABC Motsepe League.

Wakala aliyefanikisha Humud kusaini Real Kings amesema kwamba ana matumaini mchezaji huyo atafanya vizuri Afrika Kusini.

Humud ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars na Zanzibar Heroes amejiunga na timu hiyo baada ya mkataba wake kumaliza na Coastal Union ambayo kwasasa imeshuka daraja.

Real Kings kwasasa inawania nafasi ya kupanda daraja ili iweze kushiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini msimu ujao ambapo imeamua kujihiimarisha kwa kusajili wachezaji tofauti kwenye kikosi hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *