Mwanamuziki wa Bongo fleva, Abdukiba amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haoni sababu ya kazi zao kama kundi na kaka yake kuanza kutoka kutokana na Alikiba kuwa na kazi nyingi za kushirikiana hivyo atasikika kwa muda mrefu katika kazi mbalimbali.

Abdu Kiba amesema kutokana na Alikiba kuwa na kazi nyingi sana hivyo ameona yeye saizi bora atoke na Mr. Blue ili kuleta utofauti maana Alikiba atakuwa amesikika kwenye kazi nyingi sana na kushirikishwa.

Mbali na hilo Abdu Kiba alifafanua namna ambavyo watu walimwelewa vibaya baada ya kusema yupo tayari kufanya kazi na WCB Wasafi, akisema kuwa yeye anaweza kufanya kazi na WCB Wasafi kibiashara kama kufanya show, collabo lakini si kuhamia au kusimamiwa na label hiyo.

Abdu Kiba ni mwanamuziki wa Bongo fleva aliyejizolea sifa kutoakana na kazi zake kufanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio na TV.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *