Mahakama nchini Korea Kusini imemuadhibu mwanaume mmoja baada ya kumkuta na hatia ya kusambaza uzushi kuwa mjane wa rais wa zamani wa nchi hiyo anapanga kufunga ndoa na mtayarishaji nguli wa muziki kutoka Marekani, Dr. Dre.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa alidai katika uzushi huo kuwa mjane huyo, Lee Hee-ho anataka kufunga ndoa na Dr. Dre ikiwa ni mpango wake wa kutakatisha fedha za rushwa alizoachiwa na mumewe, Kim Dae-jung.

Mahakama ya wilaya nchini humo ilimpa adhabu ya kulipa faini ya dola elfu nne ($4,400) baada ya kumkuta na hatia ya kumvunjia heshima Rais aliyefariki dunia na mjane wake.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Lee Eun-hee ilieleza kuwa inalenga kuwa fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na usambazaji wa uzushi unaolenga kuwahafua viongozi na watu wengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *