Staa wa Muziki nchini Marekani, 50 Cent anatarajia kuigiza kwenye filamu ya Gerard Butler iliyopewa jina ‘Den Of Thieves’.

Kwenye filamu hiyo 50 Cent ataigiza kama mwizi wa benki huku Butler ataigiza kama polisi mlaa rushwa ambaye anakiuka haki za raia.

Filamu ya Den Of Thieves inaanza kurekodiwa Atlanta na Georgia nchini Marekani na inatarajiwa kutoka mwaka 2018 baada ya kukamilika.

Staa huyo anaungana na mastaa wenzake kama vile Ludacris na Tyrese ambao wameigiza kwenye filamu ya Fast na Furious ambazo hadi sasa zimefikia namba saba huku namba nane ikitarajiwa kutoka mwakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *