Staa wa Hip-Hop nchini Marekani, Tyga ameingia matatani mara baada ya Jaji wa mahakama moja nchini humo kutaka akamatwe na aadhibiwe ikiwezekana kupewa kifungo jela.

Jaji huyo amesema mwanamuziki huyo ikiwezekana aadhibiwe ili iwe fundisho kwa wengine kutokana na kukaidi amri ya mahakama hiyo iliyomtaka afike kusikiliza kesi inayomkabili.

Staa huyo alitakiwa kufika mahakamani hapo jana kujibu tuhuma zinazomkabili kuhusu kudaiwa kutolipa pesa za pango la nyumba kwa mmiliki wa nyumba hiyo.

tyga

Baada ya Tyga kukaidi agizo la mahakama hiyo jaji aliyekuwa akiongoza kesi hiyo alivitaka vyombo vya usalama kumkamata mwanamuziki huyo na kumfikisha mahakamani hapo huku akiwaomba wajumbe wa baraaza la mahakama wajadili adhabu ikiwezekana kumhukumu aende jela kutokana na dharau kubwa aliyoionesha kwa mahakama.

Tyga ambaye kwa sasa ameshahama kwenye nyumba hiyo anadaiwa pia pesa kwa ajili ya uharibifu alioufanya kwenye nyumba hiyo wakati alipokuwa akiishi baada ya kuharibu geti linalojiongoza lenyewe (automatic gate) na vigae vya bafuni.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *