Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza bei ya viingilio katika mechi ya marudiano kundi A kombe la Shirikisho kati ya Yanga SC na MO Bejaia kutoka Algeria.

 Viingilio vitakuwa Sh 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko ya viti vya kijani, bluu na chungwa wakati viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000.

Wakati viti vyenye hadhi ya daraja A kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 kwa mujibu wa waratibu wa Yanga.

Kikosi cha watu 35 ambao ni wachezaji na viongozi wa MO Bajaia kutoka Algeria, wamewasili Dar es Salaam Agosti 9 kwa ajili ya mechi hiyo ya marudiano.

Yanga wataikabili MO Bejaia katika mchezo wa nne wa hatua ya nane bora kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaofanyika Jumamosi Agosti 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *