Staa wa Bongo movie upande wa filamu za mapigano, Jimmy Mponda  maarufu kama J.Plus anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la “The Foundation” hivi karibuni.

 J.Plus amesema Kwanza anamshukuru Mungu kwa uzima, ukimya wake haukuwa wa nia mbaya bali ni katika harakati za kuboresha kazi zake, na kuangalia nini awaletee mashabiki wake ili waridhike

 Staa huyo amesema kwenye filamu hiyo mpya “The Foundation” amecheza na Inspector Seba na anafikiri itarudisha heshima ya movie za mapigano nchini Tanzania ambapo kwasasa tasnia hiyo imeonekana kushuka.

J.Plus amesema ameamua kurejea tena katika ulingo wa filamu ili kuitetea tasnia hiyo kwasababuc ameona kama ina legea legea na huenda  ikapoteza ubora kwa mashabiki wa filamu hizo nchini.

J.Plus ni miongoni mwa waigizaji bora nchini ambapo amewahi kutamba na filamu zake kama vile Misukosuko, Jamal na Double J baada ya kufanya vizuri katika tasnia ya filamu za mapigano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *