Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amechaguliwa kuwania tuzo kwenye tuzo za vijana 100 wa Bara la Afrika wenye ushawishi mkubwa (100 Most Influential Young Africans).

Alikiba amechaguliwa kwenye tuzo hizo akiwa ni mtanzania pekee atakayewania tuzo hizo za vijana wenye ushawishi mkubwa.

Tuzo hizo utolewa kwa vijana wenye ushawishi wanaoweza kuwahamisha vijana wengine wa Afrika kufanikisha malengo yao na kufanikiwa katika maisha kama walivyofanikiwa wao katika sekta mbalimbali.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake ‘Seduce Me’ ambao umekuwa gumzo nchini pamoja na bara la Afrika kwa ujumla baada ya kufikisha views milioni 2 ndani ya siku tatu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *