Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Job Ndugai ameishukuru kambi rasmi ya upinzani kwa changamoto walizokuwa wakimpatia wakati wa shughuli za bunge zikiendelea.
Spika Ndugai ametoa shukrani hizo wakati akitoa shukrani mbalimbali kwa wabunge na Mawaziri na watu mbalimbali waliokuwa nae bega kwa bega wakati bunge likiendelea.
Ndugai amesema kuwa “Kambi rasmi ya upinzani asanteni sana kwa changamoto ambazo mmetupatia mara kwa mara zimetusaidia sana katika kuendesha shughuli hapa, na sema asanteni sana na tuendelee na utaratibu huo kwasababu kwa kweli kwa pamoja tunaweza,”.
Bunge limehairishwa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuendelea hadi tarehe 5 Septemba mwaka huu.