Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, P. Diddy ameongoza orodha ya wanahip hop walioingiza mkwanja mrefu baada ya kuwa na utajiri wa jumla ya $820m (£633m) kulingana na jarida la Forbes.

Forbes wamesema utajiri wake ulioimarishwa na mikataba ya kibiashara ambayo alitia saini na Diageo kwa ajili ya Ciroc vodka na mavazi yake ya Sean John.

Lakini rapa na produsa Jay Z alipanda hadi nafasi ya pili sana kutokana na uwekezaji wake wa $200m (£155m) katika kampuni ya kuuza muziki mtandaoni ya Tidal.

jay-z-performance

Jay Z

Pia ana mvinyo kwa jina Armand de Brignac, na anamiliki pia lebo ya Roc Nation ndiyo chanzo cha mapato yake.

Mwaka uliopita, utajiri wa Diddy ulikuwa $750m (£579m) na wa Jay Z $610m (£471m).

Forbes waliandaa orodha yao wakizingatia mapato ya miaka ya nyuma pamoja na stakabadhi za kifedha, thamani ya mali inayomilikiwa na wanamuziki hao na pia kwa kuzungumza na wachanganuzi, mawakili, mameneja na wataalamu wengine katika tasnia ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *