Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM, Adam Mchomvu ametumia ukurasa wake wa Instagram kumtia moyo Vanessa Mdee ambaye anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

mdee

Adam Mchomvu A.K.A Baba Johnii amemtia moyo mwanamuziki huyo na kumwambia avumilie hali aliyo nayo kwa sasa kwani hawezi kufa bali atakomaa kiaskari.

Vanessa Mdee ni miongoni mwa wanamuziki wa Bongo Fleva waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wanaojihisisha na uuzaji wa dawa za kulevya ambao walitakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *