Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amewasili nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo tarehe 25 – 26 Februari mwaka huu kwa ajili ya shughuli za kiserikali.

Museveni amekuja Tanzania kwa mara ya kwanza toka Serikali ya Awamu ya tano chini uongozi wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli yenye kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu iingie madarakani mwaka 2015.

Rais huyo wa Uganda amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Baadae Museven akapata nafasi ya kukagua gwaride pamoja na kukipigiwa mizinga ya kumkaribisha nchini Rais huyo mkongwe nchini Uganda.

Rais huyo yupo nchini kwa shughuli mbali mbali za kidiplomasia zinazoguasa nyanja za kiuchumi, Biashara na ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *