Baada ya Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kutangaza matokeo ya kidato cha pili na darasa la nne ambapo mkoa wa Mtwara umekuwa mkoa wa mwisho kwa matokeo hayo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza wizara mbili kubaini nini tatizo la kufeli kwa mkoa wa Mtwara.

Waziri mkuu ameziagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda kubaini sababu zilizosababisha shule 9 kati ya 10 zilizofeli kwenye matokeo ya kidato cha pili zimetokea mkoani humo.

mtwara

Hayo ameyasema jana wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo Mpanda kwaajili ya kufungua duka la dawa katika Bohari ya dawa (MSD) mkoani humo.

Waziri mkuu amesema haiwezekani mkoa uwe na shule 9 ziko chini, lazima kuna tatizo, kwahiyo wizara husika ziende Mtwara zikajue kuna nini, shule 9 kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko.

Siku chache baada matokeo ya kidato cha pili shule 9 za mkoa wa Mtwara ziliongoza kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *