Klabu ya Chelsea ya Uingereza imemtambulisha rasmi kocha wake mpya, Antonio Conte kwenye mkutano wa waandishi wa habari unaondelea kwenye uwanja wa timu hiyo jijini London.

Kupitia mkutano huop na waandishi wa habari, tayari Conte amemuhakikishia nahodha wa Chelsea John Terry kuendelea kushikilia wadhifa huo.

Conte amechukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha wa sasa wa Manchester United, Jose Mourinho aliyetimuliwa kibarua cha kuinoa Chelsea miezi kadhaa baada ya kuiwezesha kutwaa ubingwa wa EPL kwenye msimu wa 2014/2015.

Blues: Antonio Conte akionyesha jezi ya Chelsea melee ya waandishi wa habari
Blues: Antonio Conte akionyesha jezi ya Chelsea melee ya waandishi wa habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *