Zuchu na Nandy nani kuibuka na tuzo

0
55

Wanamuziki wa kike wa Bongo Fleva, Zuchu na Nandy wamewekwa kipengele kimoja katika kugombe tuzo za Afrimma zitakazotolewa mwaka huu nchini Marekani.

 

Zuchu na Nandy wanachuana kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, ambapo kwenye mitandao ya kijamii, wameonekana kuwagawa mashabiki wa burudani Bongo.

 

Mbali ya Zuchu na Nandy, kwenye kipengele hicho cha Msanii Bora wa kike, wapo pia wasanii mbalimbali ndani ya Afrika Mashariki akiwemo Nadia Mukami (Kenya), Tanasha Donna (Kenya), Maua Sama (Tanzania), Rosa Ree (Tanzania), Vimka (Uganda) na wengine wengi.

 

Mchuano huo unaonekana kuwa kabambe Bongo baina ya Nandy na Zuchu, kufuatia wasanii hao kuachia nyimbo kali hivi karibuni, zinazoonekana kupendwa na kuwa na mashabiki wengi.

 

Nandy anatamba na kibao chake cha Acha Lizame alichomshirikisha Harmonize, huku Zuchu akitamba na kibao chake cha Nisamehe.

 

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Novemba 15, mwaka huu katika jiji la Dallas, Texas, nchini Marekani na kuhudhuriwa na wasanii kibao maarufu.

LEAVE A REPLY