Zuchu kusimamia mziki wake peke yake

0
38

Msanii wa muziki Bongo, Zuchu amesema Diamond Platnumz ameshamueleza kuwa kuna wakati atamuacha na ataanza kusimamia muziki wake pekee yake.

Ameeleza hayo akiongea na kipindi cha Mgahawa cha Wasafi FM ambapo pia amesema mwaka huu utakuwa wa kazi zaidi kutoka kwake baada ya mwaka jana kutambulishwa.

Boss wangu Diamond aliniambia nitakupa platform lakini kuna muda utafika nitakuacha ujitegemee mwenyewe, ujitengeneze, ukue na uji-brand mwenyewe” amesema Zuchu.

Aliendelea kwa kusema, “Mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa kutambulishwa, lakini mwaka huu ni mwaka wa kazi tu, nataka nifanye kazi kiasi kwamba nikifika sehemu sihitaji nitambulishwe tena kama zuchu wa Tanzania, nataka kutambulishwa kama Zuchu msanii mkubwa Duniani”.

LEAVE A REPLY