Zuchu azidi kufanya vizuri kwenye muziki

0
104

Mwanamuziki kutoka lebo ya muziki ya WCB, Zuchu anazidi kufanya vizuri toka atambulishwe rasmi kama msanii wa lebo hiyo kubwa ya muziki nchini Tanzania kutokana na kufanya vizuri.

Zuchu ameingia kwenye 10 bora ya wasanii waliotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube kwa mwezi April 2020 kutokana na ubora wa kazi zake.

Zuchu ameshika namba 6 akiwa ameangaliwa na jumla ya watazamaji Milioni 7.6. Katika orodha hiyo Diamond anaoza kwa kutazamwa mara Milioni 40.3.

Mwanamuziki mwengine wa lebo hiyo Rayvany anafuata akiwa nafasi ya pili akiwa na watazamaji Milioni 17.8 na namba 3 ni Harmonize akiwa ametazamwa mara Milioni 16.3

LEAVE A REPLY