Zuchu azidi kufanya vizuri kimataifa

0
43

Wimbo wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu uitwao Litawachoma umeingia nafasi ya 83 kwenye orodha ya video za muziki zinazotazwa dunia nzima kupitia YouTube.

Orodha hiyo ni kwa mujibu wa mtandao wa ChartsAfrica na kusema kuwa wimbo hao kwasasa unafanya vizuri katika mtandao wa Youtube kutokana na ubora na uzuri wa wimbo huo.

Zuchu ameshare nasi taarifa hizo zilizopistiwa kupitia ukurasa wa ChartsAfrica uliopo Twitter, na pia amewashukuru mashabiki zake kwa kumsapoti katika kazi zake.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Zuchu ameandika ‘Nimeamka na habari njema Video ya Wimbo wetu pendwa Litawachoma ft Diamond Platnumz uko namba 83 kwenye on trending youtube ulimwenguni Thank you so much to each one of you my beautiful supporters And thank you to Billboard Charts Africa for the recognition”.

Zuchu ni msanii anayefanya vizuri toka atambulishwe katika lebo ya muziki ya WCB chini ya Diamond Platnumz mapema mwaka huu.

LEAVE A REPLY