Zitto Kabwe akamatwa na Polisi akiwa nyumbani kwake leo asubuhi

0
195

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii.

Zitto Kabwe amekamatwa akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam  na amepelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe.

Taarifa fupi iliyotolewa na Afisa habari wa Chama hicho Abdallah Khamis, amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo.

Afisa habari huyo amebainisha kwamba sababu za kukamatwa kwake zinawezekana kuwa ni kutokana na hotuba yake aliyoitoa juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa mdogo wa madiwani kwenye kata 43 nchini.

LEAVE A REPLY