Zidane: Mechi ya leo si ushindani kati ya Ronaldo na Neymar

0
167

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema mchezo wa leo ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu yake na PSG sio ushindani wa Ronaldo na Neymar bali ni mchezo wa timu mbili.

Zidane ameongeza kuwa hawezi kuzuia watu kuongelea nyota hao wawili kwani wanakutana mchezaji ghari zaidi ulimwenguni na mchezaji bora duniani kwa hiyo kunakuwa na sababu ya ziada ya watu kuongea lakini hawachezi peke yao.

 Zidane pia amesema wao kama Madrid licha ya kutokuwa na msimu mzuri lakini hawana presha na mchezo huo na wanafurahia kucheza aina hiyo ya mechi.

Real Madrid inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga ikiwa nyuma kwa alama 17 dhidi ya vinara Barcelona wenye alama 59.

LEAVE A REPLY