Zari: Sina mpango wa kutembea na mwanaume wa kitanzania tena

0
357

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amesema kuwa hataweza kutembea na mwanaume wa Kitanzania tena.

Kauli ya Zari imekuja baada ya kuacha na Diamond ambao walikuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.

Zari alimwaga Diamond mapema mwaka huu siku ya wapendanao baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Lakini pia Zari ameibuka na kudai kuwa mtoto wake  Tiffah sio wa Tandale hii iliyokea siku chache zilizopita wakati Zari na marafiki zake walipokuwa Kwenye Instagram live.

Zari alifunguka na kusema mtoto wake Tiffah anashindwa kutofautisha kati ya R na L tabia ambayo ameirithi kutoka kwa Upande wa Baba yake kwani Watanzania wengi hawawezi kutofautisha R na L na wengi wao wanamuita Zali badala ya zari.

LEAVE A REPLY