Zari awatahadharisha mashabiki wake na matapeli

0
55

Aliyekuwa na mpenzi wa Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady amejitokeza kutoa tahadhari baada ya watu kuibuka na kutapeli watu kupitia jina lake na sura yake

Akizungumza kupitia video aliyoipost Instagram Zari amesema kuwa kumekuwa kuna kundi la watu wanatapeliwa kupitia jina lake.

Watu hao wamekuwa wakiambiwa kuwa Zaria anafanya mafunzo ya biashara za sarafu mtandaoni Forex na wengine hutumia jina lake kuomba msaada kupitia taasisi yenye jina lake kwaajili ya kusaidia watu.

Zari amesema “Nahitaji mfahamu sifanyi biashara, sifanyi Forex, sijaomba pesa kuwezesha taasisi yangu ya Zari Foundation. Sipeleki watu nje ya nchi kuwatafutia kazi.

Watu wengi wamekuwa wakitapeliwa na lawama zinarudi kwangu kwasababu matapeli wamekuwa wakitumia sura yangu”.

LEAVE A REPLY