Zari awajibu waliomwita mshamba

0
79

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari the Bosslady amefunguka juu ya wanaomuita mshamba baada ya kupost picha akiogelea nyumbani kwake.

Mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram ameandika kuwa aachwe na maisha yake, kwani kama wakiona hawawezi kutazama picha zake basi waondoke katika mtandao huo.

“Sijawahi ona mtu anaogelea na dera, sijui ni mimi tu au?. Mniache na ushamba wangu wa Kiganda na nyie mbaki na ujanja wa Kibongo, na mtaendelea kuona picha zangu za hivi kila wikiendi kwani haya ni maisha yangu”.

Zari ameamua kuandika hivyo baada ya kuibuka mijadala mtandaoni kuhusu picha zake hizo alizoweka jana Jumapili akiwa ameonekana kuvalia mavazi ya ufukweni.

LEAVE A REPLY