Zari atupa dongo kwa mpenzi mpya wa Diamond

0
100

Mzazi mwenziye staa wa Bongo Fleva, Diamond, Zari The Boss Lady amedaiwa kutupa madongo ya gizani kwa watu wanaomchokonoa kuhusu mpenzi mpya wa Diamond, Tanasha Donna.

Kuna baadhi watu wamekuwa wakimsema mitandaoni kuwa ameachana na Diamond lakini bado anamuonea wivu kwa jinsi anavyojiachia na Tanasha.

Kwa kuonesha kwamba anawajibu kwa siku za hivi karibuni, Zari ameonekana kuandika jumbe huku akitupia picha mbalimbali za bata zake ambazo mashabiki wengi wa mrembo huyo wamezitafsiri kwamba anawajibu wale wanaomchimba kuhusu mpenzi wake wa zamani (Diamond) kuchukuliwa na Tanasha.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Comment za wenye hasira ziwe fupi…. kwa nini maisha ya mtu yanakuumiza hivyo bana? Fanya yako…,” aliandika Zari katika moja ya posti zake Instagram.

LEAVE A REPLY