Zari ampiga dongo Diamond

0
103

Aliyekuwa mwanamuziki wa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ ameibuka na kumtupia dongo zito mzazi mwenzake huyo na kusema hana pesa.

Zari na Diamond walikuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne na walifanikiwa kuzaa Watoto wawili Lakini Penzi Lao liliingia shubiri mapema mwaka jana Baada ya Diamond kuchepuka na Hamisa na kuzaa naye mtoto.

Tangu waachane sio siri Diamond na Zari hawajawahi kuwa na mahusiano mazuri na siku ya Leo ameweka wazi kuwa Diamond hana pesa kama watu wengi wanavyosema.

Zari alifunguka hayo alipoulizwa na shabiki kama Diamond asingekuwa tajiri na maarufu basi Zari asingeweza kuwa naye kwenye mahusiano, Swali ambalo Zari alijibu kuwa Diamond hana pesa.

LEAVE A REPLY