Zari amchana Diamond kisa kushindwa kuwaona watoto

0
353

Aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amemshambuliwa kwa maneno  Diamond baada ya kushindwa kwenda kuwaona waoto wake nchini Afrika Kusini.

Zari amemshambulia Diamond kupitia snapchat, muda mfupi kabla hajaelekea kanisani yalionekana yakihusishwa na ujumbe ambao Diamond aliuandika kwenye Instagram kuhusu wanawake.

Zari amemkosoa kwa kushindwa kuwaona watoto wake kwa muda mrefu kinaonesha kuwa anayezungumziwa ni baba Tifah.

Baadaye, Zari aliweka picha inayomuonesha akiwa mbele ya kioo na nguo nyingi na kuandika ujumbe kuwa ni muda wa kanisani.

Zari ameandika  “Mameneja wengine wanapaswa kuhakikisha ubora kabla wasanii wao hawajaweka upuuzi kwenye mitandao ya kijamii kwa kupata kiki kivyovyote… hivi ni lini mara ya mwisho umewaona wanao.. Nina amini wamesahau yote kuhusu wewe mpuuzi…. fikiria kabla ya kuandika kwenye picha. Mjinga.”

Zari alitangaza kuachana na Diamond, akaiachia rasmi funguo za ikulu ya WCB ya Madale na kuhamia nchini Afrika Kusini.

LEAVE A REPLY