Zari akanusha kurudiana na Diamond

0
855

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amekanusha taarifa za kurudiana na mwanamuziki huo baada ya kuachana.

Kufuatia video ya wimbo wa msanii wa bongo fleva nchini Diamond kutoka akiwa amemshirikisha Rayvany na kibao chao cha Iyena kumekuwa na mvumo wa maneno mengi yakidai kuwa kuonekana kwa Zarinah Hassan katika video hiyo kumedhihirisha wazi kuwa wawili hao wamerudiana.

Zari kupitia ukurasa wake wa instagram ameamua kuzima uvumi huo kwa kuweka wazi kuwa uhusiano uliopo kati yake na baba watoto wake, Diamond Platinumz ni kama wazazi tu na si vinginevyo.


Amesema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya watoto wao hivyo mashabiki wao waelewa hivyo na kwamba wanawapenda sana.

Katika mahusiano yao Zari na Diamond walijaliwa kupata watoto wawili ambao ni Tiffah na Nillan. Zari ndiye aliyetangaza kuvunja mahusiano na Diamond kwa kile alichodai muimbaji huyo alikuwa akimvunjia utu wake kwenye mitandao.

LEAVE A REPLY