Zari afunguka mipango yake baada ya kuachana na Diamond

0
570

Baada ya kuachana na Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amefunguka na kusema kuwa ataendelea na biashara zake kama zamani na atorudiana na mwanamuziki huyo tena.

Zari amesema kuwa ameamua kuendelea na biashara zake kwani alikuwa anafanya baishara hizo kabla ya kuwa katika mahusiano na Diamond.

Zair amesema kuwa anaendelea na maisha yake ya kuandaa matamasha mbali mbali na hivi karibuni anatarajia kuja na reality show yake inayokwenda kwa jina la Life of Zari The Boss Lady.

Zari amesema kinachoendelea ni ukweli mtupu na kabla ya kutangaza uamuzi wake wa kumuacha Diamond walikaa wiki tatu bila kuzungumza.

Mrembo huyo kutoka Uganda ameendelea kusema kuwa ameamua kuachana na Diamond kutokana na tabia yake ya kutembea na wanawake hovyo hivyo ameamua kumuacha huru afanye anavyotaka.

Zari aliamua kuachana na Diamond siku ya sikukuu ya wapendanao ‘Valentine Day’ ambapo ameamua kauadika yake moyoni kupitia mtandao wa kijamii.

LEAVE A REPLY