Zanzibar: Mtumishi wa TRA atiwa mbaroni kwa kulawiti mtoto wa miaka 13

0
300

Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar linamshikilia Mtumishi wa TRA, Hassan Abuutwalib maarufu kama Kiringo kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye miaka 13

Kiringo alimpeleka mtoto huyo katika nyumba iliyokuwa haijamalizwa kujengwa huko Fuoni Uwandani ambapo alimlawiti baada ya kumpa dawa za kupoteza fahamu

Mtoto huyo alipata maumivu makali ambapo ripoti ya uchunguzi wa madaktari ilithibitisha kuathirika sehemu za siri za nyuma za mtoto huyo

Kamanda wa Polisi Nasiri amesema ameunda timu ya uchunguzi iliyojumuisha wakuu wa upelelezi wa wilaya tatu Wilaya ya Mjini, Wilaya ya Magharibi A na B kufanya uchunguzi juu ya suala hilo zito.

Kiringo alishawahi kushutumiwa kwa matukio tofauti ya kulawiti kabla ya hili na sasa jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahujiano zaidi.

LEAVE A REPLY