Zambia: Wapinzani wakata rufaa ya matokeo ya uchaguzi

0
101

Chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kimeandika lalamiko kwa mahakama kuu nchini humo kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita ambayo yalimchagua tena kwa rais Edgar Lungu.

Chama cha United Party for National Development kimedai kuwa uhesabuji wa kura za uchaguzi mkuu wa mapema mwezi huu ulikuwa na dosari hivyo wameomba kuhesabiwa upya kwa kura hizo.

Rais Lungu ambaye ametetea kiti chake alitarajia kuapishwa siku ya Jumanne baada ya kupata ushindi wa 50.35% ambao ulimuwezesha kukwepa urudiwaji wa upigwaji kura.

Lalamiko hilo la wapinzani linakubaliwa na katiba ya Zambia hivyo kuapishwa kwa rais Lungu kutasubiri uamuzi wa mahakama wa iwapo uhesabuji wa kura utarudiwa au ushindi wa Bw. Lungu utathibitishwa.

Hata hivyo tume ya uchaguzi ya Zambia imesisitiza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Mgombea urais wa upinzani, Hakainde Hichelema, ambaye alipata 47,6% ya kura zote ameliambia shirika la utangazaji la BBC kuwa uchaguzi umepokonywa mikononi mwake na matokeo hayaakisi mwitikio na mapokeo ya watu waliokuwa wakimuunga mkono wakati wa kampeni.

Katiba ya Zambia inaipa Mahakama ya katiba ya Zambia wiki mbili kutoa uamuzi juu ya lalamiko la uchaguzi.

LEAVE A REPLY