Z Anto afunguka kufungwa kwa binti kiziwi

0
218

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Z-Anto amesema kuwa jambo la kukamatwa kwa Bi. Kiziwi lilikuwa baya kwa sababu hakutegemea katika maisha yake.

Z-Anto amesema kuwa B. Kiziwi alivyoambiwa anafungwa miaka 8 akili ilimruka hadi akawa anapewa dawa za usingizi wakati yupo jela.

Z- Anto amesema kuwa “Tatizo kubwa ambalo lilimpoteza uraiani alikamatwa na madawa ya kulevya nchini China, akafungwa kwa takribani miaka nane ndiyo amekuja kukanyaga tena Tanzania mwishoni mwa mwaka 2019, japokuwa kila mtu alikuwa anaongea lake na wengine walikuwa wanatamani atoke”.

Aidha msanii huyo ameendelea kusema “Alivyokuwa jela nilikuwa nawasiliana naye kwa njia ya simu kila mwezi, alikuwa ananihadithia maisha yake ya kule, mazingira na anavyoendelea”.

Pia amesema mrembo huyo Sandra Khan maarufu kama Binti kiziwi, alikuwa mke wake wa ndoa kabisa japokuwa walikuja kuachana kwa makosa binafsi, na miaka mitatu baada ya kuachana kwao ndiyo akasikia amekamatwa.

LEAVE A REPLY