Yusuf Mlela hana tatizo na wasanii wa muziki kuigiza

0
7

Mwanamuziki wa Bongo Movie, Yusuf Mlela amesema kutokana na mabadiliko yanayohitajika kwenye sanaa, haoni tatizo wasanii wa Bongo Fleva wakiingiza kwenye filamu na tamthiliya.

 

Mlela ambaye ukiachilia mbali na uigizaji pia ni muongozaji wa tamthilia, amesema kuwa sanaa kila siku inatakiwa ikue ndiyo maana wasanii wengi wa Bongo Fleva wameamua kufanya hivyo.

 

“Unajua sanaa inatakiwa ikue kila siku mambo yanatakiwa mapya, ukiangalia sisi wote ni wasanii na msanii lazima aweze kuonyesha uwezo wake katika sanaa, acha waingie ili kuleta vitu vya tofauti,” alisema Mlela.

 

Wasanii wa Bongo Fleva walioingia kwenye uigizaji ni pamoja na Nandy, Billnass na Quick Racka ambao wanafanya vizuri katika baadhi ya tamthilia.