Young Killer aweka wazi sababu ya kuwa na mlinzi wa kike

0
360

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Killer amefunguka na kusema kuwa ameamua kulindwa na mlinzi wa kike kwasababu ameridhishwa na uwezo wake wa kushiriki mapambano.

Rapa huyo amempa ajira mwanamke mmoja kuwa mlinzi wake binafsi, baada ya kuridhishwa na uwezo wake wa kushiriki mapambano makali.

Young Killer amesema kuwa uamuzi wake haukuwa ‘kiki’ na kwamba lilianza kama wazo kuwa angependa awe na mlinzi binafsi wa kike, na wazo lake likakamilika baada ya rafiki yake mmoja kumpendekezea mwanamke ambaye alikubaliana na uwezo wake.

Kwasasa Young Killer anatembea na mwanamke huyo ambaye pamoja ni kwamba ni mzuri ila tabasamu lake ni adimu kuliona mana yupo kikazi kweli.

Mwanamuziki huyo amekuwa mtu wa kwanza mwanaume maarufu Tanzania kuwa na mlinzi binafsi mwanamke anayezunguka naye sehemu mbalimbali.

 

LEAVE A REPLY