Young Killer akiri kuachana na mpenzi wake

0
850

Baada ya tetesi kuzagaa za kuachana na mpenzi wake, hatimaye msanii wa  hip hop Bongo, Young Killer amekiri kugombana na mpenzi wake Halimaty Msodoki.

Msodoki ambaye amedumu kwenye mahusiano na mpenzi wake huyo tangu alipoanza kujulikana kwenye game ya Bongo Fleva.

Young Killer amesema kuwa kwa sasa mrembo ‘Miss Hip Hop’ amerudi kwao Mwanza kwa mambo yake binafsi.

Mwanamuziki huyo pia amesema kuwa jamii inapaswa kutambua kwamba maswala ya mahusiano huwa yana mambo mengi ikiwemo ugomvi.

Pia mwanamuziki huyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kwani anatarajia kauchia ngoma kali siku za karibuni.

LEAVE A REPLY