Young Killer afunguka sababu ya kuondoka Wanene

0
96

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Killer amefunguka na kusema kuwa ameamua kuachana na lebo ya Wanene Entertainment kwasababu amemaliza mkataba wake na leo hiyo.

Young Killer ameweka wazi kuwa baada ya kuisha kwa mkataba wake hakutaka kusaini tena na labo hiyo kwa sababu kwa muda ambao amefanya nao kazi kuna matarajio aliyategemea ndani ya kampuni hiyo lakini hakufanikiwa kupata.

Kutokana na hayo mwanamuziki huyo ameamua kuachana na lebo hiyo kwakuwa alichokuwa anatafuta  amekosa ameona ni bora alipokuwa anafanya kazi akiwa mwenyewe.

Young Killer aliweka wazi kuwa moja kati ya mambo aliyokuwa anayatarajia lakini hakuyaoni ni pamoja na kukuza wigo wa muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania.

Young Killer amesema pamoja na kuondoka katika label hiyo yupo tayari kufanya kazi na label nyingine endapo tu atapendezwa na mkataba atakaopewa.

LEAVE A REPLY