Young Dee na Tunda wamaliza tofauti zao

0
102

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Young Dee amemaliza tofauti yake na video vixen, Tunda baada ya wawili hao kuonekana pamoja siku za hivi karibuni.

Wawili hao wameonekana pamoja kwa siku ya kwanza katika mitandao ya kijamii kwa kuweka picha yao ya pamoja waliokuwa kwenye gari ambapo mashabiki wao wameonekana kufurahi jambo hilo.

Young Dee na Tunda waliwahi kuwa maadui sana kwa kipindi kirefu baada ya wawili hao kushindwa kuwa pamoja kimapenzi na kugombana hivyo kila mmoja kufanya ustaarabu wake huku wakirushiana maneno ya chinichini.

Tunda na Young Dee kuwepo pamoja kunaweza kuashiria urudi kwa mahusiano yao kwasasa baada ya wawili hao kuonekana pamja.

Wawili hao wameanza kuonekana pamoja baada ya Tunda kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Castro Dickson ambaye ni mtangazaji wa Siz Kita kinachorushwa Clouds Tv.

Si Young Dee wala Tunda ambaye ameelezea ukaribu wao wa sasa kama wamerudisha penzi lao kama hapo awali au ni marafiki tu wa kawaida.

LEAVE A REPLY