Young Dee kuachia mixtape mwishoni mwa mwaka huu

0
291

Staa wa Bongo fleva, Young Dee amesema kwamba anatarajia kuachia mixtape yake mwaka huu.

Young Dee amedai kuwa yeye na uongozi wake wa MDB wamejadiliana na kuona kuna umuhimu wa kuanza kutoa nyimbo nyingi kwaajili ya mashabiki katika mfumo wa mixtape.

Staa huyo pia amesema nyimbo zipo nyingi sana halafu alikuwa kimya walifikiria mwishoni mwa mwaka huu watengeneze platform ambayo watu wataweza kupata ngoma zake online na zitakuwa katika mfumo wa mixtape.

Rapa huyo amesema tayari ameanza kuandaa kazi mpya kwaajili ya mixtape hiyo na baadaye ndipo watatangaza lini itatoka kabla ya mwaka huu kuisha.

LEAVE A REPLY