Young Dee amlilia Agnes Masogange

0
377
Young Dee

Baada ya mwili wa Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kuzikwa jijini Mbeya, msanii wa Bongo Fleva, Young Dee amesema marehemu alikuwa mtu wa watu.

Young Dee alisema kipindi cha uhai wake, Masogange alikuwa ni mtu wa watu ambaye alikuwa hapendi ugomvi na hajawahi kusikia akigombana na mtu japo yeye hajawahi kufanya naye kazi.

Amesema kuwa “Japo sijawahi kufanya naye kazi, lakini alikuwa mtu wa watu kwani sijawahi kusikia akigombana na mtu yeyote, kwa sasa wasanii tuendelee kumuomba Mungu na tuachane na maovu pia tuwe wamoja kwani hujui lini utakufa,”.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita kwenye Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua Ugonjwa wa Nimonia na upungufu wa damu mwilini na kisha kuzikwa juzi Jumatatu.

LEAVE A REPLY