Yaya Toure atemwa kikosi cha klabu bingwa

0
273
MANCHESTER, ENGLAND - MAY 24: Yaya Toure of Manchester City applauds supporters as he is replaced during the Barclays Premier League match between Manchester City and Southampton at Etihad Stadium on May 24, 2015 in Manchester, England. (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amemuacha kiungo Yaya Toure kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya kombe la klabu bingwa msimu mpya wa mwaka 2016-17.

Yaya Toure hakujumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 17 kitakachoshiriki michuano hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Toure mwenye umri wa miaka 33 hatoichezea  City kwenye mechi hizo za klabu bingwa hatua ya makundi ambapo watakutana dhidi ya Borussia Monchengladbach, Celtic and Barcelona.

Gurdiola ameonesha kutovutiwa na Yaya Toure toka atue kwenye klabu hiyo ya Manchester City baada ya kuanza kumuacha kwenye mechi ya mchujo ya klabu bingwa dhidi ya Steua Bucharest ya nchini Romania ambapo City ilishinda 5-0 ugenini.

Yaya Toure inaonekana hana bahati na kocha huyo kwani aliwahi kumfundisha wakati alipokuwa Barcelona na kuamua kummuza Manchester City ambapo sasa hamtaki tena kwenye klabu hiyo.

Kocha huyo toka atue kwenye klabu hiyo wachezaji wangi wameoneshwa nja ya kutokea kutokana na kutovutiwa na viwango vyao pamoja na kutokuwa katika mipango yake meneja.

Wachezaji walioachwa kwenye kikosi hicho ambapo wengine wamepelekwa kwa mkopo na wengine kuuzwa kabisa ni Mangala aliyejiunga Valencia, Samir Nasri aliyejiunga Sevilla, Willyfred Bonny aliyejiunga Stoke City pamoja na Joe Hart aliyejiunga Torino ya Italia.

LEAVE A REPLY