Yanga yazindua Jarida maalum

0
237

Klabu ya Yanga imezindua rasmi Magazine yake inayoelezea habari za klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijni Dar es Salaam.

Yanga imezindua magazine hiyo ikiwa imesalia siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Simba SC ikiwa na lengo la kujiongezea kipato.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wa klabu ya Yanga hapo jana imeeleza kuiingiza rasmi sokoni Magazine hiyo hii leo siku ya Ijumaa.

Tunapenda kuwataarifu wanachama, mashabiki na wadau mbalimbali wa soka kuwa ‘Yanga Magazine’, itaanza kuuzwa rasmi kesho (Ijumaa) kuanzia saa 3:00 Asubuhi Makao Makuu ya Klabu.

LEAVE A REPLY