Yanga yaomba msaada wa vifusi kwaajili ya uwanja wao

0
131

Klabu ya Yanga kupitia msemaji wake Dismass Ten imefunguka na kuomba msaada kwa wadau mbalimbali wa soka nchini kuwasaidia vifusi vya mchanga ili waweze kurekebisha kiwanja chao cha Kaunda kilichopo Jangwani, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo Dismass amesema kulingana na ukubwa wa uwanja huo wanahitaji watu ambao wataweza kujitolea ili waweze kukamilisha zoezi la ujenzi.

Dismass amesema wanakarabati uwanja huo kwa maelekezo mazuri kutoka kwa wataalamu wa ujenzi ili timu yao iweze kupata sehemu ya kufanyia mazoezi.

“Bado tunahitaji kifusi kwa ajili ya ujenzi huu kwa sababu eneo ni kubwa, wale wote ambao wanaweza kutusaidia kwenye eneo hili tunawakaribisha kutokana wanayanga wanahitaji kujenga Yanga yao, kwa maana timu iweze kupata sehemu maalum ya kufanyia mazoezi. Pia niwashukuru wale ambao wameshaanza kutusaidia katika hili kwa namna moja ama nyingine”,.

 Klabu ya Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho, kuwavaa Mtibwa Sugar katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara huku ikimkosa mchezaji wake wa Kimataifa, kiungo Tshishimbi Kabamba anayetumikia adhabu ya kukosa mechi moja baada ya kupata kadi 3 za njano katika mechi 3 zilizopita.

LEAVE A REPLY