Yanga SC yaingia kambini kwa ajiri ya maandalizi dhidi ya Medeama ya Gahana

0
210

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC imeingia kambini katika hoteli ya Tiffany jijini la Dar es Salaam kwa ajiri ya maandalizi ya mechi ya marudiano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama FC ya Ghana.

Yanga ianatarajia kurudiana na Medeama Jumatano ya Julai 27, mwaka huu katika uwanja wa Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi nchini Ghana.

Katika mechi ya kwanza iliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijinI Dar es Salaam Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 na Medeama.

TP Mazembe ya Jamhuri ya Kongo inayoongoza kundi hilo inatarajia kuikaribisha timu ya Mouloudia Olympique Bejaia “MO Bejaia” mjini Lubumbashi.

TP Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi ikiwa na alama saba, ikifuatiwa na MO Bejaia ikiwa na alama tano, Medeama ina alama mbili na Yanga ikiwa na alama moja.

LEAVE A REPLY