Yanga kuondoka Jumamosi kuelekea nchini Ghana

0
391

Yanga SC inatarajia kuondoka nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya mechi ya marudiano ya mashindano ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama Julai 27 mwaka huu.

Msafara wa klabu hiyo utakuwa na jumla ya watu 30 wakiwemo wachezaji 20 na viongozi 10 unatarajiwa kuondoka siku ya jumamosi.

Yanga imeingia kambini katika hoteli ya Tiffany iliyopo jiji la Dar es Salaam kwa ajiri ya maandalizi ya mchezo huo utakaofanyika katika uwanja wa  Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi nchini Ghana.

Yanga kwa sasa inafanya mazoezi yake katika uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY