Wolper: Wivu muhimu kwenye mapenzi

0
47

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa, hakuna kitu kizuri kama wivu kwenye uhusiano wa kimapenzi, kwani ndiyo unaoleta hamasa kwenye mahusiano.

Wolper amesema kuwa ukimuona mwenza wako haonyeshi wivu juu yako ujue akupendi kabisa hivyo wivu ni kitu muhimu sana kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Wolper alisema kuwa, kuna watu wengine hawapendi kabisa mambo ya wivu kwenye mahusiano yao, lakini kwa upande wake, anaona wivu una umuhimu sana.

Pia amesema kuwa katika mahusiani yake yote aliyokuwa nayo alionyesha wivu ili kumlinda mpenzi wake asichukuliwe na mwanaume mwingine.

Muigizaji huyo amesema kuwa “Mimi bila wivu itakuwaje jamani, naona kama hakuna mapenzi vile, maana raha uulizwe uko wapi, uko na nani, nitaku peleka hakuna kwenda mwenyewe; hayo ndiyo mambo ya kwenye mapenzi,”.

LEAVE A REPLY