Wolper: Wanaume wametufanya madaraja

0
111

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacque­line Wolper amesema kuwa wanaume wamekuwa wakiwafanya wasa­nii wa kike kama madaraja ya mafanikio yao.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kupotea kwa ndoa za wasanii wa kike nchini tofauti na wasanii wa kiume ambapo kila kukicha wanafunga.

Wolper amedai kuwa wasanii wengi wa kike mawazo ya kuolewa yameshafutika mioyoni mwao kwa sababu wanaume wengi wamekuwa waki­watumia kama madaraja.

Wolper amesema kuwa mara ny­ingi wanaume wamewachuku­lia wasanii kama daraja la kusonga mbele au kukuza majina yao lakini siyo mapenzi ya dhati.

Miaka ya hivi karibuni, wasanii wengi wa kike wamekuwa wakizalishwa na kulea watoto wao peke yao, baada ya kuachwa na wanaume zao.

Ikumbukwe kuwa muigizaji huyo alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki, Harmonize kabla ya kuwa na jina kubwa lakini baada ya kujuliakana alimwana na kuchukua mwanamke mwingine.

LEAVE A REPLY